06. Maimamu kuweni kati na kati


Swali 6: Baadhi ya maimamu wa misikiti katika Ramadhaan wanarefusha katika du´aa na baadhi ya wengine wanafupiza. Ni lipi jambo la sawa?

Jibu: Sahihi ni kwamba kusiwe na uchupaji mpaka wala uzembeaji. Urefushaji ambao unawatia matatani watu umekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofikiwa na khabari kwamba Mu´aadh bin Jabal amewarefushia watu wake swalah alighadhibika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ghadhabu ambayo hajapatapo kamwe kughadhibika mfano wake katika mawaidha na akamwambia:

“Je, wewe ni mfitini, ee Mu´aadh?”[1]

Kinachotakikana ni mtu afupike juu ya maneno yaliyopokelewa au azidishe kidogo pasi na kuwatia uzito. Hapana shaka kwamba kurefusha kunawatia uzito watu na kuwapatisha dhambi na khaswa wale madhaifu katika wao. Wako watu ambao ni wafanya biashara wanaokuwa nyuma yake na hawapendi kumaliza swalah kabla ya imamu na inakuwa uzito kwake kubaki pamoja na imamu.

Kwa hivyo nasaha zangu kwa ndugu zangu maimamu wawe kati na kati. Kadhalika anatakiwa baadhi ya nyakati kuacha kusoma Qunuut ili wale wasiokuwa na elimu wasifikiri kuwa kukunuti ni jambo la lazima katika Witr.

[1] al-Bukhaariy (704) na Muslim (972).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 13
  • Imechapishwa: 11/04/2021