07. Sababu ya sita ya maisha mazuri: Kukumbuka neema za Allaah

6- Kusimulia neema za Allaah za nje na za ndani. Hakika kuzitambua na kuzisimulia ni njia moja wapo ambayo Allaah anaondosha mawazo na misononeko. Sambamba na hilo kunamuhimiza mja juu ya kushukuru, jambo ambalo ni ngazi ya hali ya juu kabisa. Haijalishi kitu hata kama mja yuko katika hali ya umasikini, maradhi au mtihani aina nyingine. Hakika akilinganisha kati ya neema za Allaah juu yake ambazo hawezi kuzidhibiti na wala kuzihesabu na yale yenye kuchukiza yaliyomfika, basi haviwezi kulingana kwa asilimia ndogo kabisa. Bali wakati Allaah anapomjaribu mja kwa kumsibu kwa majanga mbalimbali yanayochukiza ambapo mtu huyo akatekeleza jukumu la subira, kuridhia na kujisalimisha, basi jambo lake huwa jepesi na uzito wake unakuwa mwepesi. Matumaini ya mja kwa ule ujira wake, thawabu zake na kumwabudu Allaah kwa kule kutekeleza kazi ya kusubiri na kuridhia, basi huyafanya mambo machungu yakawa matamu ambapo utamu wa thawabu zake zikamsahaulisha ule uchungu wa kusubiri kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 21
  • Imechapishwa: 15/06/2020