Anachotazama mposaji kwa yule mwanamke anayemposa

Swali: Ni mambo gani ambayo yameruhusiwa kwa mposaji kuyatazama kutoka kwa yule anayemposa wakati anapoomba kumtazama?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Lililo salama zaidi katika haya ni kwamba inatosha kutazama uso, viganja vya mikono na miguu. Akitazama nywele hakuna ubaya pia. Kwa sababu nywele wakati mwingine zinaonekana kwa wale wanamme ambao ni Mahram zake na mume. Kwa hiyo hakuna neno. Lakini akitosheka kutazama uso wake, viganja vyake vya mikono na miguu yake hakuna neno. Akitazama nywele pia hakuna ubaya. Kwa sababu nywele zinaweza kuonekana katika baadhi ya nyakati.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4134/ما-مقدار-ما-يراه-الخاطب-ممن-يريد-خطبتها
  • Imechapishwa: 14/06/2020