… na Mitume Wake… – Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanamini Mitume wote na kwamba Allaah ametuma Mitume. Mtume wa kwanza ni Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aadam pia (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ni Mtume kwa kizazi chake. Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mitume wote ni haki. Mitume wote wamefikisha ujumbe wa Allaah. Mitume wote wametumwa kwa lengo la kuwalingania watu katika: kumuabudu Allaah peke Yake na kumtii. Sambamba na hilo wanawatahadharisha shirki na maasi. Mitume wote hii ndio ilikuwa kazi yao kuanzia wa mwanzo wao Aadam mpaka wa mwisho wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

 

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com