… na Vitabu Vyake… – Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini Vitabu vyote vya Allaah alivyoteremsha kwa Mitume. Wanaamini vile walivyovijua kama Tawraat, Injiyl, Zabuur na Qur-aan. Vilevile wanaamini vile wasivyovijua kwa njia ya ujumla. Amesema (Ta´ala):

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ

“Kwa yakini Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa hoja bayana na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na mizani.” (57:25)

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini kuwa Allaah ameteremsha Vitabu kwa Mitume na kwamba ni haki. Wanaamini vilevile kuwa Vitabu hivyo ni katika maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Miongoni mwa Vitabu hivyo ni pamoja vilevile na Tawraat, Injiyl, Zabuur na Qur-aan. Hivi ni miongoni mwa Vitabu alivyoteremsha.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com