08. Sababu ya Nuuh (صلى الله عليه وسلم) kuitwa kuwa ndio Mtume wa kwanza

Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameitwa kuwa ndio Mtume wa kwanza kwa sababu yeye ndiye alikuwa Mtume wa kwanza kwa waliokuwa katika ardhi baada ya kutokea shirki. Kabla ya hapo walikuwa katika Tawhiyd wakifuata Shari´ah ya Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Baada ya hapo ndipo kukatokea shirki katika watu wa Nuuh (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu ya kuvuka kwao mipaka kwa Wadd, Suwaa´, Yaghuuth na Nasr[1]. Hapo ndipo Allaah akawatumia Nuuh ili awalinganie katika kumuabudu Allaah peke Yake na kuwatahadharisha na kumshirikisha. Pale walipoendelea na hawakuitikia ndipo Allaah akawaangamiza. Tunamuomba Allaah afya.

[1] Tazama “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy (4920).

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com