07. Kinywaji cha mnywaji pombe Motoni

C- Kunywa maji ya usaha ya watu wa Motoni. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameahidi kwamba yule mwenye kunywa pombe basi atamnyweshwa kutoka katika asili ya wazimu.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nini hiyo asili ya wazimu?” Akasema: “Ni jasho la watu wa Motoni”, au “Usiri wa watu wa Motoni.”[1]

Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wangu ameapa kwa ufalme Wake: Mja wangu hatokunywa glasi ya pombe isipokuwa Nitamnywesha badala yake maji yenye moto ya Motoni, ni mamoja aliadhibiwa au alisamehewa.”[2]

Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

 “Yule mwenye kufa ilihali ni mnywaji pombe, basi Allaah atamnywesha kutoka kwenye mto wa Ghutwah.” Kukasemwa: “Ni nini mto wa Ghutwah?” Akasema: “Ni mto unaopita kutoka kwenye nyuchi za makahaba.” Harufu mbaya inayotoka kwenye nyuchi zao itawaudhi watu wa Motoni.”[3]

Hapo kale alikuweko mlevi mmoja ambaye alipita karibu na kijiji kilichokuwa na kiwango kikubwa cha pombe ambapo akasoma mashairi yafuatayo:

Tiyzanaabaad zipo zabibu

kila ninapopita karibu hushangazwa

na wale wanaokunywa maji

Tahamaki akasikia sauti inayotoka chini ya mti ikisema:

Na Motoni yapo maji;

mtenda maasi hatokunywa glasi hata moja

isipokuwa matumbo yake yatayeyuka

[1] Muslim (2002).

[2] Ahmad (5/257).

[3] Ahmad (4/399) na Ibn Hibbaan (5346).

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 16-18
  • Imechapishwa: 22/07/2020