07. Faida ya kwanza baada ya kujua yaliyotangulia

Faida ya kwanza: Kufurahi kwa fadhilah na rehema za Allaah. Tunachomaanisha ni kwamba midhali Allaah amekujaalia elimu hii, basi unatakiwa kufurahi kwa ajili ya rehema na fadhilah za Allaah. Fadhilah za Allaah kwa sababu amekuongoza katika Uislamu. Rehema Zake kwa sababu amekujaalia kuwa mmoja katika wao. Fadhilah za Allaah kwa sababu amekujuza Uislamu na akakuongoza kwao. Rehema Zake kwa sababu amekujaalia kuwa mmoja katika wao. Amesema (Ta´ala):

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Zake, basi kwa hayo wafurahi. Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.”[1]

Unafurahi kwa kuona Allaah amekifungua kifua chako, Allaah amekufunza, Allaah amekufahamisha dini Yake, Allah amekuongoza na kukuhurumia mpaka ukawa mmoja katika waislamu hao. Hii ni neema kubwa.

[1] 10:58

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 23
  • Imechapishwa: 12/10/2021