06. Wenye kiu na wenye muumbuko

2- Adhabu za Aakhirah zimegawanyika aina mbalimbali:

A- Kiu siku ya Qiyaamah. Qays bin Sa´d bin ´Ubaadah amepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mwenye kunywa pombe atapatwa na kiu siku ya Qiyaamah.”[1]

´Abdullaah bin ´Amr amesema:

“Katika Tawraat imekuja: “Pombe ladha yake ni chungu. Allaah ameapa kwa ufalme Wake na kusema: “Yule mwenye kuinywa baada ya kuiharamisha basi nitampiga kiu siku ya Qiyaamah.”[2]

B- Kufanywa muumbuko na mbaya siku ya Qiyaamah. al-Ajurriy amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesema:

“Usimsalimie mnywaji pombe, msiwatembelee wanapokuwa wagonjwa na wala msihudhurie mazishi yao. Hakika mnywaji pombe atakuja siku ya Qiyaamah upande mmoja wa mashavu yake yamepinda na macho yake yamepiga bluu, ulimi wake utaning´inia juu ya kifua chake na mate yake yanatiririka juu ya tumbo lake. Kila mwenye kumuona atashikwa na kinyaa.”[3]

Moja katika mapokezi ya Ahmad yanasema kuwa haitakiwi kumswalia mwenye kufa hali ya kuwa ni mnywaji pombe.

[1] Ahmad (3/422).

[2] al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (10/222).

[3] Ameipokea al-Bukhaariy 805/2308) ikiwa ni cheni ya wapokezi pungufu kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr:

”Usimsalimie chapombe.”

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 25/07/2020