Anayoweza kudhihirisha mwanamke mbele ya baba na mtumwa wake

2868- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna neno juu yako – si vyenginevyo ni baba na mtumwa wako tu.”

Ameipokea adh-Dhwiyaa´ katika ”al-Mukhtaarah” kupitia kwa Abu Daawuud, kutoka kwa Abu Jaamiy´ Saalim bin Diynaar, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambaye amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja kwa Faatwimah na mtumwa ambaye alikuwa amemzawadia. Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa na kanzu ambayo, pindi anafunika kwayo kichwa chake basi haifiki miguuni mwake, na pindi anapofunika miguu yake, haifiki kichwani mwake. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoona hali aliyomo akasema: ”Hakuna neno juu yako – si vyenginevyo ni baba na mtumwa wako tu.”

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

Katika Hadiyth kuna dalili ya wazi kabisa kwamba inafaa kwa mwanamke kuonesha kichwa na miguu yake mbele ya baba yake na mtumwa wake. Ndani yake kuna Radd kwa Abul-A´laa al-Mawduudiy (Rahimahu Allaah) ambaye amesema waziwazi kwamba haitakiwi kwa mwanamke kuonesha uso na miguu yake mbele ya baba yake, ami yake, kaka yake, mtoto wake wa kiume mpaka wanawake mfano wake[1]!

[1] al-Hijaab, uk. 289-290

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/869)
  • Imechapishwa: 21/07/2020