28 – Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Hakiym amenikhabarisha, kutoka kwa Shu´ayb: al-Layth ametukhabarisha, kutoka kwa Yaziyd bin al-Haad, kutoka kwa Ibraahiym bin Sa´d, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan bin Zayd, kutoka kwa Muhammad bin Sa´d bin Abiy Waqqaas, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:
”´Umar aliomba idhini ya kuingia kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa amezungukwa na wanawake wa ki-Answaar. Walikuwa wakizumgumzisha na wakimuuliza maswali mengi hali ya kuzinyanyua juu sauti zao. Wakati ´Umar alipoomba idhini wakaharakisha kujisitiri. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa idhini ya kuingia na huku akaanza kucheka. ´Umar akasema: ”Allaah akuchekeshe meno yako, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: ”Nashangazwa na wanawake hawa ambao walikuwa kwangu. Wakati tu waliposikia sauti yako wakakimbilia haraka kujisitiri.” ´Umar akasema: ”Wewe una haki zaidi ya kuogopwa, ee Mtume wa Allaah!” Kisha ´Umar akasema: ”Enyi maadui wa nafsi zenu! Mnaniogopa mimi na wala hamumuogopi Mtume wa Allaah?” Wakasema: ”Ndio. Wewe ni mshupavu na mkali zaidi kuliko Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake hujashika njia isipokuwa shaytwaan atashika njia nyingin mbali na ile utayoshika.”[1]
[1] Ahmad (1/171), al-Bukhaariy (3294) na Muslim (2396).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 43
- Imechapishwa: 06/09/2026
28 – Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Hakiym amenikhabarisha, kutoka kwa Shu´ayb: al-Layth ametukhabarisha, kutoka kwa Yaziyd bin al-Haad, kutoka kwa Ibraahiym bin Sa´d, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan bin Zayd, kutoka kwa Muhammad bin Sa´d bin Abiy Waqqaas, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:
”´Umar aliomba idhini ya kuingia kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa amezungukwa na wanawake wa ki-Answaar. Walikuwa wakizumgumzisha na wakimuuliza maswali mengi hali ya kuzinyanyua juu sauti zao. Wakati ´Umar alipoomba idhini wakaharakisha kujisitiri. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa idhini ya kuingia na huku akaanza kucheka. ´Umar akasema: ”Allaah akuchekeshe meno yako, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: ”Nashangazwa na wanawake hawa ambao walikuwa kwangu. Wakati tu waliposikia sauti yako wakakimbilia haraka kujisitiri.” ´Umar akasema: ”Wewe una haki zaidi ya kuogopwa, ee Mtume wa Allaah!” Kisha ´Umar akasema: ”Enyi maadui wa nafsi zenu! Mnaniogopa mimi na wala hamumuogopi Mtume wa Allaah?” Wakasema: ”Ndio. Wewe ni mshupavu na mkali zaidi kuliko Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake hujashika njia isipokuwa shaytwaan atashika njia nyingin mbali na ile utayoshika.”[1]
[1] Ahmad (1/171), al-Bukhaariy (3294) na Muslim (2396).
Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 43
Imechapishwa: 06/09/2026
https://firqatunnajia.com/06-umar-akishika-njia-shaytwaan-anapita-njia-nyingine/