23 – Nuswayr bin al-Faraj amenikhabarisha: Shu´ayb bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Abiy Salamah: Muhammad bin al-Munkadir ametuhadithia, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Niliota jinsi ninavyoingia Peponi. Nikaona kasri nyeupe ambayo kwenye ua wake alikuwemo kijakazi amesimama. Nikasema: ”Ni ya nani hii, ee Jibriyl?” Akasema: ”Hii ni ya ´Umar bin al-Khattwaab.” Nikataka kuingia ndani nitazame, lakini nikakumbuka wivu wako.” Akasema: ”Namtoa fidia mama yangu na baba yangu, ee Mtume wa Allaah! Nikuonee wivu wewe?”[1]
24 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr, kutoka kwa Jaabir na Ibn-ul-Munkadir, kutoka kwa Jaabir, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Niliingia Peponi na nikaona ndani yake kasri nyeupe, au nyumba. Nikasema: ”Ni ya nani hii?” Wakasema: ”Ni ya ´Umar bin al-Khattwaab.” Nikataka kuingia ndani, lakini nikakumbuka wivu wako, ee Abu Hafsw, hivyo sikuingia.” ´Umar akalia na kusema: ”Nikuonee wivu wewe, ee Mtume wa Allaah?”
25 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: al-Mu´tamir ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Umar ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin al-Munkadir, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Niliingia Peponi na nikaona kasri ya dhahabu. Nikasema: ”Ni ya nani hii?” Wakasema: ”Bwana mmoja anayetokana na Quraysh.” Hakuna kilichonizuia kuingia ndani, ee bwana wa Khattwaab, isipokuwa ni kutokana na ule wivu wako ninaojua.” Akasema: ”Nikuonee wivu wewe, ee Mtume wa Allaah?”
26 – ´Aliy bin Hujr ametukhabarisha: Ismaa´iyl ametuhadithia: Humayd ametuhadithia, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Niliingia Peponi na nikaona kasri ya dhahabu. Nikasema: ”Ni ya nani kasri hii?” Wakasema: ”Ni ya kijana mmoja anayetokana na Quraysh.” Nikafikiri mtu huyo ndiye mimi, ndipo nikasema: ”Kwani ni nani?” Wakasema: ”´Umar bin al-Khattwaab.”
27 – ´Amr bin ´Uthmaan ametukhabarisha: Muhammad bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa az-Zubaydiy, kutoka kwa az-Zuhriy… ´Amr bin ´Uthmaan pia amenikhabarisha na kusema: Baqiyyah ametuhadithia, kutoka kwa az-Zubaydiy: az-Zuhriy amenikhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:
”Pindi tulipokuwa tumeketi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: ”Wakati nilipokuwa nimelala nilijiona niko Peponi. Tahamaki mwanamke mmoja alikuwa akitawadha pembezoni mwa kasri. Nikasema: ”Ni ya nani kasri hii.” Wakasema: ”Ya ´Umar.” Nikakumbuka wivu wake, nikageuka na kwenda zangu.” ´Umar, ambaye naye alikuwa katika kikao hicho, akalia na kusema: ”Nikuonee wivu wewe, ee Mtume wa Allaah?”
[1] al-Bukhaariy (3242) na Muslim (2395).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 41-43
- Imechapishwa: 06/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 41-43
Imechapishwa: 06/09/2026
https://firqatunnajia.com/05-kasri-ya-umar-peponi/