Swali 6: Mwanamke akipata tone la damu ndogo mchana wa Ramadhaan na damu hii ikaendelea mwezi mzima wa Ramadhaan ilihali ni mwenye kufunga. Je, swalah yake ni sahihi?

Jibu: Ndio, swawm yake ni sahihi. Tone hili si lolote kwa sababu ni yenye kutoka katika mshipa. Kuna Athar kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba amesema:

”Hakika tone ambalo linakuwa kama damu yenye kutoka puani si hedhi.”

Haya ndio yanayosemwa juu yake (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 11
  • Imechapishwa: 12/06/2021