Upande wa kulia wa safu au wa kushoto?

Swali: Nimesikia fatwa ikisema kwamba upande wa kulia wa safu – hata kama utakuwa mbali na imamu – ni bora kuliko upande wa kushoto – hata kama upande huo wa kushoto uko karibu zaidi na imamu. Nikasikia fatwa nyingine ilio kinyume na hiyo ya kwanza inayosema kwamba upande wa kushoto wa imamu ukiwa karibu ndio bora kuliko upande wa kulia ikiwa uko mbali. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba upande wa kulia wa safu ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah na Malaika zake wanawasifu walioko upande wa kuliani mwa safu kwa walimwengu walioko juu.”

Sitambui msingi unaosema kuwa ikiwa upande wa kushoto uko karibu ndio bora. Jambo hilo linajitaji dalili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 12/06/2021