Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

13 – Ni Mwenye kusifika milele juu ya sifa Zake kabla ya kuumba Kwake.

14 – Sifa Zake hazikuongezeka kutokana nao.

15 – Kama ambavyo siku zote alikuwa ni mwenye kusifiwa kwa sifa Zake, vivyo hivyo ndivo atavoendelea kuwa milele.

16 – Hakuwa ni Muumbaji baada ya kuumba wala Mwanzilishi viumbe baada ya kuanzisha viumbe.

17 – Alikuwa na sifa ya uungu wakati hapakuwa yeyote wa kuabudu, alikuwa ni Muumbaji wakati hapakuwa kiumbe yeyote[1].

18 – Kama ambavyo anazingatiwa ni Mwenye kuwahuisha wafu na amestahiki jina hili kabla ya kuwapa uhai, kadhalika amestahiki jina la Muumbaji kabla ya kuwaumba.

[1] Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy amesema:

“Maana yake ni kwamba Allaah (Ta´ala) alikuwa ni Mwenye kusifiwa Mola kabla ya kuwepo wenye kulelewa, Muumba kabla ya kuwepo viumbe.” (Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 116)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Maaniy´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 11/11/2021