Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

9 – Hafanani na viumbe/watu[1].

10 – Yuhai na hafi, Msimamizi wa kila kitu Asiyelala.

11 – Muumbaji asiyekuwa na haja, mtoaji riziki bila matatizo[2].

12 – Mwenye kufisha bila ya khofu yoyote, Mwenye kufufua bila ya uzito wowote.

[1] Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy amesema:

“Makusudio sio kukanusha sifa, kama wanavofanya Ahl-ul-Bid´ah. Abu Haniyfah amesema katika “Fiqh-ul-Akbar”:

“Hafanani na chochote katika viumbe Wake na hakuna chochote katika viumbe Wake kinachofanana Naye.”

Kisha baada ya hapo akasema:

“Sifa Zake zote zinatofautiana na sifa za viumbe. Anajua, lakini si kama ujuzi wetu, na Anaweza, lakini si kama uwezo wetu, Anaona, lakini si kama kuona kwetu.” (Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 85)

[2] Si mwenye kuhisi ugumu wala kutilia bidii.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Maaniy´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 22
  • Imechapishwa: 11/11/2021