06. Hapa ndipo utazingatiwa umelingania kwa Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

3 – Kuilingania.

4 – Kusubiri juu ya maudhi yatakayompata mtu ndani yake.

MAELEZO

1 – Allaah akikutunuku elimu na ukaifanyia kazi, basi ni itakulazimu uwalinganie watu katika kheri hii ambayo Allaah amekutunuku. Hivyo uwalinganie watu kumuamini Allaah, waamini majina, sifa na matendo Yake na waamini uola Wake na waamini kuwa Yeye pekee ndiye anastahiki kuabudiwa.

Vilevile unatakiwa kulingania kumuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uamini kuwa yeye ni Mtume, kwamba ndiye Mtume wa mwisho na kwamba hakuna Mtume mwingine baada yake, kwamba ametumilizwa kwa majini na watu wote.

Aidha ulinganie katika dini ya Uislamu, uwalinganie watu wampwekeshe Allaah na wamnyenyekee kwa kumtii, wajitenge mbali na shirki na washirikina, watekeleze maamrisho na wajiepushe na makatazo Yake. Hapo utazingatiwa umelingania kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 18
  • Imechapishwa: 01/02/2023