Dhambi uliyofanya ikiwa ulimpiga mtu na mfano wa hayo [tawbah yake] nenda na umwache na yeye akupige kama jinsi ulivompiga. Ikiwa ulimpiga mgongoni naye akupige mgongoni, ikiwa ulimpiga kichwani naye akupige kichwani au sehemu nyingine yoyote uliyompiga na yeye ajilipize. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا

“Na malipo ya uovu ni uovu mfano wake.” (42:40)

فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ

Basi atakayekufanyieni uadui, basi nanyi mfanyieni uadui kwa kadiri alivyokufanyieni uadui.” (02:194)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/89)
  • Imechapishwa: 01/02/2023