Kutubu kwa dhambi ya kumsengenya mtu

Kuhusiana na kumsengenya na kumsema mtu vibaya wakati ambapo alikuwa hayupo, hili wametofautiana wanachuoni [namna ya kutubia].

Kuna ambao wamesema ni lazima umwendee na kumwambia kuwa umemsema vibaya mbele ya watu, hivyo ninakuomba unisamehe na unikwamue [katika hali hii].

Wanachuoni wengine wakasema kuwa usimwendee, bali hilo lina upambanuzi. Ikiwa alijua kuwa ulimsengenya, ni lazima umwendee na mtafute ufumbuzi. Ikiwa hakujua, usimwendee. Muombee msamaha kwa Allaah na mseme kwa mazuri yake kwenye kikao ambapo ulimsengenya. Hakika mema yanafuta maovu. Maoni haya ndio sahihi zaidi. Kuhusiana na usengenyi ikiwa uliyemsengenya hakujua kama ulimsengenya, unatosha kumtaja kwa uzuri mbele ya kikao ulipomsengenya na kumuombea msamaha kwa Allaah kwa kusema:

“Ee Allaah! Msamehe.”

Kama ilivokuja katika Hadiyth:

“Kafara ya uliyemsengenya ni kwa kumuombea msamaha.”

Tawbah  ni lazima urudishe haki kwa wenye nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/90)
  • Imechapishwa: 01/02/2023