05. Hapa ndipo utazingatiwa umeifanyia kazi elimu yako

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

2 – Kuifanyia kazi.

MAELEZO

Bi maana kuifanyia kazi ile elimu iliyotangulia. Haitoshi kule kumjua kwako Allaah kwa majina, sifa na matendo Yake, kumjua kwako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuijua kwako dini ya Uislamu. Bali ni lazima ufanyia kazi vile inavyopelekea elimu hii.

Kufanyia kazi vile unavyopelekea ujuzi wako kuhusu Mola Wako maana yake ni ufanyie kazi vile unavyopelekea utambuzi wako kuhusu majina na sifa za Allaah. Kwa msemo mwingine umthibitishie majina mazuri, pia umthibitishie sifa kuu na uamini kuwa Yeye ndiye Muumba, Mwendesha mambo, Mwenye kuruzuku, Mfalme, Mola na uamini kuwa Yeye ndiye anastahiki kuabudiwa. Huku ndio kuifanyia kazi. Unatakiwa kuamini kwa moyo wako na ufanyie kazi kwa viungo vyako vya mwili. Matokeo yake umtekelee ´ibaadah Allaah kukiwemo swalah, swawm, zakaah na hajj.

Kufanyia kazi vile unavyopelekea ujuzi wako kuhusu Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana yake ni kwamba uamini kuwa Mtume Wako ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ulazima wa kumfuata, kumtukuza, kumpenda, kusadikisha maelezo yake, kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha, makatazo yake na uhakikishe unatendea kazi kumfuata katika matendo yako yote.

Kufanyia kazi vile unavyopelekea ujuzi wako kuhusu dini ya Uislamu maana yake ni wewe kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha na kumnyenyekea kwa kumtii hali ya kufuata maamrisho Yake, kujiepusha na makatazo Yake na ujitenge mbali na shirki na washirikina.

Ukiyafanyia kazi mambo haya basi utazingatiwa umehakikisha suala la pili; kufanyia kazi vile inavyopelekea elimu yako juu ya Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na dini ya Uislamu kwa dalili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 17
  • Imechapishwa: 01/02/2023