04. Hapa ndipo utazingatiwa umemjua Mtume na Uislamu

2 – Kuhusu ujuzi wa kumtambua Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) utambue kuwa Mtume Wake ni Muhammad mwana wa ´Abdillaah mwana wa ´Abdil-Muttwalib mwana wa Haashim, Haashim anatokana na Quraysh, Quraysh wanatokana na waarabu, waarabu wanatokana na kizazi cha Ismaa´ily mwana wa Ibraahiym kipenzi mwandani wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Aidha unatakiwa kujua kuwa alitumwa kutokea Makkah, kitu ambacho mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) atakibainisha huko mbele.

3 – Kuhusu utambuzi wa dini ya Uislamu ni kwamba unatakiwa uijue dini ya Uislamu kwa dalili na si wa kwa kufuata mkumbo na kwamba Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah (Ta´ala) kwa kumpwekesha, kunyenyekea Kwake kwa kumtii na kujiepusha mbali na shirki. Uislamu umeitwa hivo kwa sababu ya kule kujisalimisha na kumnyenyekea Allaah kwa njia ya kumtii maamrisho Yake na ujitenge mbali na shirki na washirikina.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 16
  • Imechapishwa: 01/02/2023