05. Hadiyth “Swalah tano ni kifuo cha madhambi kwa yalio kati yake… “

354 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

الصلوات الخمس: كفارةٌ  لما بينها، ثم قال: رسول الله صلى الله عليه وسلم: أرأيت لو أن رجلا كان يعتمل ، وكان بين منزله وبين معتمله خمس أنهارٍ، فإذا أتى معتمله عمل فيه ما شاء الله فأصابه الوسخ أو العرق، فكلما مر بنهرٍ اغتسل، ما كان ذلك يُبقى من درنه، فكذلك الصلاة كلما عمل خطيئةً فدعا واستغفر غفر له ما كان قبلها.

“Swalah tano ni kifuo cha madhambi kwa yalio kati yake.” Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mnaonaje lau mtu angelikuwa ni mfanya kazi na kukawa na mito mitano kati ya nyumbani kwake na kazini kwake. Anapofika kazini kwake anafanya kile anachotaka Allaah ambapo anapatwa na uchafu au jasho. Kila anapopita kwenye mto ule anaoga; je, kutabaki uchafu wowote? Basi vivyo hivyo na swalah; kila anapotenda dhambi anaomba du´aa na msamaha, basi anasamehewa yale yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” na ”al-Mu´jam al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na neno. Kuna Hadiyth nyinginezo tena nyingi zinazoitia nguvu.

[1] Swahiyh kupitia zingijne.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/263)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy