Swali: Kuna fadhilah maalum zilizothibiti kufanya ´Umrah katika miezi ya hajj zinazotofautiana na miezi mingine?

Jibu: Wakati mzuri zaidi wa kufanya ´Umrah ni ndani ya mwezi wa Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”´Umrah ndani ya Ramadhaan ni sawa na hajj.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Imekuja katika upokezi wa al-Bukhaariy:

”´Umrah ndani ya Ramadhaan ni sawa na kuhiji nami.”

Bi maana pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kisha baada ya hapo kuhiji katika Dhul-Qa´dah. Kwa sababu ´Umrah zake zote (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)zilifanyika katika Dhul-Qa´dah. Amesema (Subhaanah):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah.”[1]

[1] 33:21

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/324)
  • Imechapishwa: 01/04/2023