Kukata swawm kwa kusikia adhaana au asubiri mpaka imalizike?

Swali: Je, mfungaji akate swawm pale tu atakaposikia adhaana au asubiri mpaka imalizike?

Jibu: Kukiadhiniwa basi itafaa kwake kufungua. Isipokuwa akijua kuwa muadhini amekosea. Akiwa jangwani, akasikia adhaana lakini bado anaona jua, basi asifungue mpaka jua lizame. Lakini akiwa mjini pale muadhini anapoadhini umefika wakati wa kukata swawm. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa katika kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”

Imekuja katika Hadiyth:

“Waja wanaopendeza zaidi kwangu ni wale waharakishao kukata swawm.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023