… na ndio dini ya Mitume ambao Allaah aliwatuma kwayo kwa waja Wake.

MAELEZO

Mitume wote hawakuwataka watu wakubali kuwa Allaah ndiye Mwenye kuumba, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha. Kwa kuwa wanalitambua hilo. Waliwataka watu wao wampwekeshe Allaah kwa ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)

Hawakuwataka wakubali ya kwamba Allaah ndiye Mola kwa kuwa ni wenye kulikubali hilo. Bali walichowaambia ni:

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)

Bi maana acheni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall) katika ´ibaadah.

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi niabuduni.”” (21:25)

Hakusema kwamba hapana mola wala muumba mwingine asiyekuwa Yeye. Bali alichowaambia (Subhaanah) ni:

أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi nicheni.” (16:02)

Bi maana hakuna muabudiwa mwengine wa haki asiyekuwa Yeye. Haya ndio malengo ya Allaah kuwatuma Mitume. Hakuwatuma Mitume ili wahakikishe Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Ni jambo lipo tayari. Lakini hata hivyo halitoshelezi. Uhakika wa mambo ni kwamba aliwatuma kwa ajili ya Tawhiyd-u-Uluuhiyyah ambayo ni kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah. Hii ndio dini ya Mitume kuanzia wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 12
  • Imechapishwa: 08/10/2016