4- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu swalah juu ya meli. Akasema:

“Swali kwa kusimama isipokuwa ikiwa kama utachelea kuzama.”[1]

Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa mtumzima alikuwa akijisaidia kwa kiguzo katika swalah.[2]

[1] al-Bazzaar (68), ad-Daaraqutwniy na ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy katika ”as-Sunan” (2/82). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

Faida:

Hukumu ya kuswali kuswali ndani ya ndege ni kama kuswali kwenye meli. Anayeweza aswali kwa kusimama. Vinginevyo mtu aswali kwa kukaa na kuashiria Rukuu´ na Sujuud.

[2] Abuu Daawuud na al-Haakim ambaye pamoja na adh-Dhahabiy wamesema kuwa ni Swahiyh. Nimeitaja katika ”as-Swahiyhah” (319) na ”al-Irwaa’” (383).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 69
  • Imechapishwa: 08/10/2016