05. Kuswali swalah ya usiku kwa kusimama na kwa kukaa

05- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali usiku mrefu kwa kusimama na akiswali usiku mrefu kwa kukaa. Alikuwa anaposoma kwa kukaa, anafanya Rukuu´ kwa kukaa, na anaposoma kwa kusimama, anafanya Rukuu´ kwa kusimama[1].

Wakati mwingine alikuwa akiswali kwa kukaa na hivyo anasoma hali ya kukaa. Kunapobaki katika kisomo chake kiasi cha Aayah thelathini au arubaini, anasimama na kuzisoma hali ya kusimama. Halafu anarukuu na kusujudu kisha anafanya vivyo hivyo katika Raka´ah ya pili[2].

Mwishoni mwa uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali swalah ya sunnah kwa kukaa. Hilo lilikuwa mwaka mmoja kabla ya kufa[3].

Alikuwa akikaa kwa kukunja miguu[4].

[1] Muslim na Abuu Daawuud.

[2] al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Muslim na Ahmad.

[4] an-Nasaa’iy, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake (1/107/2), ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy katika ”as-Sunan” (1/80) na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 08/10/2016