15 – Amenihadithia zaidi ya mtu mmoja, kutoka kwa Abul-Waliyd at-Twayaalisiy: ´Uthmaan bin ´Umaarah Abu Hishaam az-Za´faraaniy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah ametuhadithia kuwa Anas bin Maalik alimuhadithia:

”Faatwimah, msichana wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alikuja na vipande vya mkate kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akasema: ”Ni vipande gani hivi vya mkate, ee Faatwimah?” Akasema: ”Nimetengeneza mkate. Sikuweza kujisikia vizuri mpaka nilipokuletea vipande hivi vya mkate.” Akasema: ”Hakika hiki ndio chakula cha kwanza kilichoingia tumboni mwa baba yako tangu siku tatu zilizopita.”

16 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: Ja´far ametuhadithia: Maalik bin Diynaar ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kula mkate wala nyama akashiba isipokuwa hadharani.”

Maalik amesema:

”Nilikuwa sijui nini kinachomaanishwa na ”hadharani” mpaka nilipokutana na bedui mmoja nikamuuliza. Akasema: ”Bi maana ilikuwa ni lazima akitumie mbele ya watu.”

17 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ibraahiym ametuhadithia: Ayyuub ametuhadithia, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa ´Aliy, ambaye amesema:

”Siku moja nilifika Madiynah hali ya kuwa ni mwenye njaa kwelikweli, basi nikatoka kutafuta kazi katika viunga vya Madiynah. Nikamuona mwanamke aliyekusanya udongo na nikafikiri anataka kuumeza. Hivyo nikamwendea na nikaukata kwa ajili ya tende juu ya kila kikapu kilichojazwa. Nikajaza vikapu kumi na sita mpaka mikono yangu ikapatwa na malengelenge. Kisha nikayaendea maji na nikayatumia,  halafu nikamwendea na kumuonyesha mikono yangu. Akanipa tende kumi na sita. Nikamwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza. Tukazila kwa pamoja.”[1]

18 – Ibraahiym bin ´Abdil-Malik amenihadithia: [tupu] ametuhadithia: Hudayj bin Mu´aawiyah ametuhadithia: Kinaanah, mtumwa wa Swafiyyah, ametuhadithia, kutoka kwa Swafiyyah, mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Ee msichana wa Huyayy, una chochote?” Nahisi njaa.” Nikasema: ”Hapana, naapa kwa Allaah, ee Mtume wa Allaah!” Isipokuwa tu pishi ya unga.” Akasema: ”Kanda nayo mkate mweupe.” Nikaiweka kwenye kikaango na kuipasha moto, kisha nikasema: ”Imeokwa, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: ”Unajua kama msichana wa Abu Bakr yuko na chochote kwenye mtungi wa siagi?” Nikasema: ”Hapana, naapa kwa Allaah sijui, ee Mtume wa Allaah! Sijui.” Akaenda mwenyewe mpaka akafika nyumbani kwake na kusema: ”Je, mwenye chochote kwenye mtungi wa siagi, ee msichana wa Abu Bakr?” Akasema: ”Kidogo tu, ee Mtume wa Allaah.” Akaja mwenyewe na kukamua kile kilichokuwemo kwenye mtungi wa siagi, mpaka nikakiona kile kilichotoka pamoja na siagi. Akaweka mkono wake ndani yake, akataja jina la Allaah na kuomba baraka. Kisha akasema: ”Waite dada zako. Kwani hakika najua kuwa wanahisi kile wanachohisi.” Nikawaita na tukala mpaka tukashiba. Baadaye akaja Abu Bakr. Akaomba idhini ya kuingia ambapo tukasimama na kuondoka. Kisha baadaye akaja ´Umar. Halafu akaja mtu mwingine. Wakala mpaka wakashiba na wakabakiza chakula kinige.”[2]  

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu kwa mujibu wa al-´Iraaqiy katika “Takhriyj ´Ihyaa’ ´Uluum-id-Diyn” (3/126). al-Haythamiy amesema:

”Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy. Wanamme wake ni waaminifu.” (Majma´-uz-Zawaa-id (10/315))

[2] al-Haythamiy amesema:

”Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw”. Katika cheni ya wapokezi yuko Hudayj bin Mu´aawiyah. Ameelezwa kuwa ni mwaminifu licha ya udhaifu wake. Wapokezi wengine wote ni waaminifu.” (Majma´-uz-Zawaa-id (8/311-312))

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 36-40
  • Imechapishwa: 11/06/2023