04. Mahimizo ya kumtii mume na kumfurahisha

2 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke akiswali vitano vyake, akafunga mwezi wake, akamtii mume wake na akahifadhi tupu yake, basi ataambiwa [siku ya Qiyaamah]: “Ingia Peponi kwa mlango wowote unaoutaka.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Wanawake wenu katika watu wa Peponi: ni wale wenye mapenzi mno, wenye kuzaa sana, wenye kujipendekeza kwa waume zao ambao anapokasirika [yule mume] anakuja na kuweka mkono wake juu ya mkono wa mume wake na kusema: “Mimi leo sionji usingizi mpaka uridhie.“[2]

[1] Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake (06/184 – Ihsaan) na wengineo. al-Albaaniy ameisahihisha kutokana na nyinginezo zinazoitolea ushahidi katika “Aadab-uz-Ziffaaf”, uk. 286.

[2] Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah, uk. 287.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 12-14
  • Imechapishwa: 19/09/2022