3 – Fadhwalah bin ´Ubayd (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuna watu aina tatu usiulize juu yao; mtu ambaye amefarikiana na mkusanyiko na akamuasi kiongozi wake ambapo akafa hali ya kuwa ni muasi – usiulize juu yake, mjakazi au mtumwa ambaye amekimbia na kuacha kumtii bwana wake na mwanamke mume wake yuko mbali naye na akamtosheleza na mahitaji ya kidunia ambapo akajishaua[1] na kuzurura[2] – usiulize juu yao.”[3]

Amesmea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu watatu swalah zao hazivuki masikio yao; mja ambaye yuko katika ukimbizi mpaka arudi, mwanamke anayelala wakati mume wake amemkasirikia[4] na kiongozi anayewaongoza watu ilihali wanamchukia.”[5]

Amesmea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah hamtazami mwanamke ambaye hamshukuru mume wake wakati huohuo hawezi kujitosheleza naye [kukosa kuwa pamoja naye].”[6]

Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Napaa kwa Ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake hakuna mwanamme yeyote anayemwita mke wake kitandani ambapo akamkatalia isipokuwa Ambaye yuko juu mbinguni humkasirikia mpaka amridhie.”[7]

Muslim amepokea tena upokezi mwingine:

“Mwanamke akilala hali ya kuwa amehama kitanda cha mume wake, basi Malaika humlaani mpaka arudi.”[8]

Ndani yake imekuja katika upokezi wa tatu:

“Mwanamme anapomwita mke wake kitandani akakataa ambapo akamkasirikia, basi Malaika humlaani mpaka kupambazuke.”[9]

Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia mwanamke mmoja:

“Hakika si venginevyo [mume wako] ndiye [ufunguo wa] Pepo na Moto wako.”[10]

Kwa hiyo ambaye anamtii Allaah (´Azza wa Jall) juu ya mume wake na akatekeleza haki zake, basi mume huyo atakuwa ndio ufunguo wa Pepo yake. Kwa msemo mwingine ni kwamba mume huyo ndiye sababu ya kuingia kwake Peponi. Akienda kinyume na mume wake, basi ni ufunguo wa Moto wake.

Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mwanamke ambaye anamuudhi mume wake duniani isipokuwa mke wake katika al-Huur al-´Ayn anasema: “Usimuudhi, Allaah Akuue! Huyo kwako ni mgeni tu. Karibuni atakuacha na kuja kwetu.”[11]

[1] Akaonyesha mapambo yake kwa ajili ya machafu au vile vitangulizi vya machafu kama kuangaliwa na mfano wake.

[2] Akazurura anavotaka yeye kwa ajili ya kutaka kuleta maharibifu.

[3] al-Bukhaariy katika ”Aadab-ul-Mufrad” (590), Ibn Hibbaan (50 – Mawaarid) na wengineo. Ipo katika “as-Swahiyhah” (542).

[4] Kutokana na sababu inayokubalika katika Shari´ah kama mfano wa tabia mbaya na kutomtii.

[5] al-Bukhaariy (360) na wengineo. Ni Hadiyth Swahiyh kama alivosema Ahmad Shaakir chini yake.

[6] Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah, uk. 289.

[7] Muslim (1436).

[8] Tamko hili limepokea al-Bukhaariy (09/294 – Fath) na wengineo.

[9] al-Bukhaariy (06/314 ) na (09/294 – Fath) na wengieno.

[10] Ni Hadiyth Swahiyh itakuja huko mbele kwa ukamilifu na takhriyj yake.

[11] at-Tirmidhiy (1174), Ibn Maajah (2014) na wengineo. Ipo katika ”as-Silsilah as-Swahiyhah” (173).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 14-18
  • Imechapishwa: 19/09/2022