Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

6 – Haangamii wala hatoweki.

7 – Wala hakuna kinachokuwa isipokuwa yale ayatakayo.

8 – Mawazo hayawezi kumfikia, fahamu haziwezi kumzunguka Yeye[1].

[1] Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy amesema:

“Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Na wala hawawezi kumzunguka Yeye wote kiujuzi.” (20:110)

Mawazo ni zile dhana na fahamu ni ile elimu, hivo ndivo imetajwa katika “as-Swiyhah.” Makusudio ya Shaykh (Rahimahu Allaah) ni kwamba hakuna mawazo yawezayo kuishilia Kwake, wala hakuna elimu iwezayo kumzunguka. Hakuna anayejua namna Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alivyo isipokuwa Yeye Mwenyewe. Si vyenginevo tunamjua Yeye kwa sifa Zake – ya kwamba ni Mmoja, Aliyekamilika, hakuzaa na wala hakuzaliwa, na hakuna yeyote anayelingana au kufanana Naye.” (Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 84)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Maaniy´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 22
  • Imechapishwa: 10/11/2021