03. Uwajibu wa kila mmoja katika sisi kujifunza masuala mane

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba ni wajibu juu yetu kujifunza masuala mane:

MAELEZO

Kwamba ni wajibu – Ni kile ambacho anapewa thawabu yule mwenye kukifanya na anaadhibiwa yule mwenye kukiacha. Kitu kilichopendekezwa ni kile ambacho analipwa thawabu yule mwenye kukifanya na wala haadhibiwi yule mwenye kukiacha. Ama kitu kilichoruhusiwa ni kile ambacho hakuna thawabu kwa kukifanya wala adhabu kwa kukiacha.

Maneno yake:

”Ni wajibu.”

Kwa msemo mwingine ni kwamba kitu hicho sio katika mambo yaliyopendekezwa wala mambo yaliyoruhusiwa. Bali ni miongoni mwa mambo ya lazima kwa kila mtu. Tukiacha kujifunza masuala haya basi tunapata dhambi. Kwa sababu hii ndio shani ya wajibu. Hakusema kuwa imependekezwa kwetu au ni vizuri kwetu. Bali amesema kuwa ni wajibu kwetu. Wajibu maana yake ni kitu cha kilazima. Anapata dhambi yule mwenye kukiacha. Kwa sababu elimu haifikiwi isipokuwa kwa kujifunza. Kujifunza kunahitajia kutilia umuhimu, juhudi, wakati, kufahamu na kuudhuhurisha moyo. Huku ndio kujifunza.

Masuala mane – Bi maana makaguzi. Yameitwa masuala kwa sababu ni lazima kuyaulizia na kuyapatiliza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 15
  • Imechapishwa: 18/11/2020