03. Ni ipi hukumu ya mtu anayevua soksi kila akitawadha?

Swali 03: Ni ipi hukumu ya kuvua soksi wakati wa kila wudhuu´ kwa ajili ya usalama zaidi?

Jibu: Kitendo hicho kinaenda kinyume na Sunnah na kinafanana na matendo ya Raafidhwah ambao hawajuzishi kupangusa juu ya soksi za ngozi. Wakati ambapo al-Mughiyrah (Radhiya Allaahu ´anh) alitaka kuvua soksi za ngozi za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ziache. Nilizivaa nikiwa katika hali ya twahara” na hivyo akapangusa juu yake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/158-159)
  • Imechapishwa: 27/04/2021