Swali 02: Ni nini maana ya maneno ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupangusa baada ya kuteremshwa kwa “al-Maaidah” na maneno ya ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) “Kitabu kilitangulia kabla ya ufutaji”?

Jibu: Sijui kama yamesihi kutoka kwao (Radhiya Allaahu ´anhumaa) au hapana. ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ni miongoni mwa waliopokea Hadiyth kuhusu kupangusa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hilo linajulisha kuwa hukumu imethibiti kwake baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hukumu haiwezi kufutwa baada ya kufa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/158)
  • Imechapishwa: 27/04/2021