03 – Kumpwekesha Allaah katika majina na sifa Zake

03 – Kumpwekesha Allaah katika majina na sifa Zake

Aina hii ya Tawhiyd vilevile imejengwa juu ya misingi miwili, kama Alivyobainisha (Jalla wa ´Alaa).

1 – Kuzitakasa sifa Zake (Ta´ala) kushabihiana na za viumbe.

2 – Kuamini yale yote aliyojisifu Mwenyewe na yale aliyomsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu anatakiwa kuamini kuwa sifa hizi ni za kihakika kwa njia inayolingana na utukufu na ukubwa Wake na sio mafumbo (مجازًا). Ni jambo linalojulikana fika ya kwamba hakuna mjuzi zaidi wa kumtambua Allaah kama anavyojijua Mwenyewe. Wala hakuna ambaye anamsifu Allaah kwa kumtambua zaidi baada ya Yeye Mwenyewe kama Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema juu ya nafsi Yake Mwenyewe:

أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ

“Je, nyinyi mnajua zaidi au Allaah?”[1]

Amesema kuhusu Mtume Wake:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Na wala hatamki kwa matamanio yake. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.”[2]

Amebainisha (Ta´ala) hali ya kukanusha kufanana na viumbe aliposema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “

Wakati huohuo akabainisha kuthibitisha sifa kikweli:

وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“… Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[3]

Sentesi ya kwanza ya Aayah inafahamisha kutokanusha. Kunapata kubainika kupitia Aayah ya kwamba lililo la wajibu ni kuthibitisha sifa kihakika pasi na kufananisha na wakati huohuo kukanusha ufananishaji pasi na kupotosha. Amewabainishia viumbe ya kwamba hawawezi kumzunguka (Jalla wa ´Alaa) kiujuzi. Amesema:

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na wala wao hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[4]

[1] 02:140

[2] 53:03-04

[3] 42:11

[4] 20:110

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 10
  • Imechapishwa: 13/06/2023