02 – Kumpwekesha Allaah katika ´ibaadah

2 – Kumpwekesha Allaah katika kumwabudu

Aina hii ndio ilikuwa sababu ya magomvi kati ya Mitume na nyumati zao. Aina hii ya Tawhiyd ndio ilikuwa sababu ya Mitume kutumwa ili waihakikishe. Kwa kifupi ndio maana ya hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Tamko hili limejengwa juu ya misingi miwili: kukanusha na kuthibitisha.

Ukanushaji ni pale unapokanusha vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah. Hili linahusiana na aina zote za ´ibaadah.

Kuthibitisha ni pale unapompwekesha (Jalla wa ´Alaa) katika aina zote za ´ibaadah kwa mujibu wa zile njia zilizowekwa katika Shari´ah. Sehemu kubwa ya Qur-aan inahusiana na sampuli hii:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na miungu ya uongo.””[1]

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi Niabuduni.””[2]

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

“Basi atakayemkanusha mungu wa batili na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti.”[3]

وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ

“Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Mitume Yetu: “Je, Tulifanya badala ya Mwingi wa rehema miungu mingine iabudiwe?””[4]

قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Sema: “Hakika nimefunuliwa Wahy kwamba: “Mungu wenu wa haki ni mungu Mmoja pekee” – Je, basi simsilimu?””[5]

Kuna Aayah nyingi juu ya maudhui hii.

[1] 16:36

[2] 21:25

[3] 02:256

[4] 43:45

[5] 21:108

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 9-10
  • Imechapishwa: 13/06/2023