01 – Kumpwekesha Allaah katika matendo Yake

Kupitia tafiti za kiusomi za Qur-aan imepata kujulikana kuwa kuna aina tatu za Tawhiyd:

1 – Kumpwekesha Allaah katika uola Wake.

Aina hii ya Tawhiyd inakubaliwa na maumbile ya mtu mwerevu. Amesema (Ta´ala):

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ

“Ukiwauliza: “Ni nani kawaumba?” Bila shaka watasema: “Ni Allaah.””[1]

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

“Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini au nani anayemiliki kusikia na kuona na nani anayemtoa aliye hai kutoka maiti na anayemtoa maiti kutoka aliye uhai na nani anayeendesha mambo?” Watasema: “Ni Allaah”. Basi sema: “Je, basi hamumchi?”[2]

Pindi Fir´awn alipokanusha aina hii pale aliposema:

وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Ni nani huyo Mola wa walimwengu?”[3]

alifanya hivo tu kwa sababu ya kiburi na kujifanya ni hamnazo. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ

“Hakika umekwishajua kwamba hakuna aliyeteremsha haya isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi kuwa ni ushahidi wa kuonekana.”[4]

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا

“Wakazikanusha kwa dhuluma na kujivuna na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha.”[5]

Kwa ajili hiyo Qur-aan ilikuwa ikishuka kwa njia ya kuthibitisha aina hii ya Tawhiyd kupitia vitu vyenye kuthibitishwa. Mfano wa hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

أَفِي اللَّـهِ شَكٌّ

“Je, kuna shaka kuhusiana na Allaah.”[6]

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ

“Sema: “Je, nishike Mola mwingine asiyekuwa Allaah hali ya kuwa Yeye ni Mola wa kila kitu?””[7]

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ

“Sema: “Ni nani Mola wa mbingu na ardhi?” Sema: “Ni Allaah.””[8]

Hata hivyo aina hii ya Tawhiyd haikuwanufaisha makafiri kitu, kwa sababu hawakuwa wakimuabudu Allaah (Jalla wa ´Alaa) peke yake. Amesema (Ta´ala):

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

“Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa ni washirikina.”[9]

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.”[10]

وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.””[11]

[1] 43:87

[2] 10:31

[3] 26:23

[4] 17:102

[5] 27:14

[6] 14:10

[7] 06:164

[8] 13:16

[9] 12:106

[10] 39:03

[11] 10:18

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 8-9
  • Imechapishwa: 13/06/2023