03. Kila mmoja anatofautisha kati ya matendo ya kutaka na ya kutokutaka

Mtu anatambua kuwa pindi anapopatwa na maradhi ya kutokwa na mikojo hovyo sio jambo linalomtokea kwa kutaka kwake. Akiwa hana maradhi haya mkojo unatoka kwa kutaka kwake. Mtu anajua tofauti kati ya hali hizo mbili. Hakuna anayepinga tofauti kati ya hayo mawili. Hali kadhalika yale yote yanayomtokea mja; anajua yale yenye kutokea kwa kutaka na pasi na kutaka. Katika huruma wa Allaah (´Azza wa Jall) ni kuwa mwanaadamu anafanya mambo kwa kutaka pasi na kufanyiwa hesabu kwayo. Kama mfano wa mwenye kufanya kitu kwa kusahau au usingizini. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu watu wa pangoni:

وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ ۖوَكَلْبُهُم بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ

“Tunawagueza upande wa kulia na upande wa kushoto na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini.”[1]

Wao ndio wenye kujigeuza, lakini kwa vile mwenye kulala hafanyi kitu kwa khiyari wala haadhibiwi kwa anachokifanya ndipo Allaah (Ta´ala) akakinasibisha kitendo hicho Kwake mwenyewe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusahau wakati amefunga na akala au kunywa, aikamilishe swawm yake. Hakuna mwingine isipokuwa Allaah ndiye kampa chakula na kumnywesha.”

Kula na kunywa huku amekunasibisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa kuwa kitendo hicho kimepitika kwa kusahau. Kwa hiyo haya yanakumbushia matendo yanayotokea pasi na kutaka. Sote tunajua tofauti ya maumivu yanayokuwa bila ya khiyari na mawazo yenye kuenea ambayo hatujui sababu yake ni nini na maumivu, au furaha, ambayo inatokamana na kitu cha khiyari. Hili ni jambo liko wazi na himdi zote ni za Allaah.

[1] 18:18

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/217-218)
  • Imechapishwa: 25/10/2016