Sisi tunatilia umuhimu jambo la elimu na tunajishughulisha kujifunza nayo kupitia kwa wanachuoni hawa na wengineo mfano wao.

Tunasoma vitabu vya Hadiyth kama mfano wa vitabu vya misingi Swahiyh-ul-Bukhaariy, Swahiyh-ul-Muslim, Sunan Abiy Daawuud, Sunan at-Tirmdihiy, Sunan Ibn Maajah, Sunan an-Nasaa´iy na vitabu vyake vinavyovitolea maelezo vinavyotambulika. Vilevile tunatilia umuhimu vitabu vya Tafsiri ya Qur-aan kama mfano wa cha Ibn Jariyr, al-Baghawiy, Ibn Kathiyr na Ibn Sa´diy. Pia tunatilia umuhimu kusoma vitabu vya ´Aqiydah ya Salafiyyah kama mfano wa vitabu kwa jina la “as-Sunnah” kwa ujumla wake, “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Ibn Khuzaymah na “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab  na pia tunasoma vitabu vyake vyengine vyote (Rahimahu Allaah). Vivyo hivyo tunasoma vitabu vyengine vyote vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim. Vilevile tunatilia umuhimu vitabu vya maimamu wa Da´wah kuanzia Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab mpaka hii leo. Wanachuoni wa Da´wah hii leo ni wale ambao tumewaashiria punde kidogo.

Tunasoma vitabu vya Fiqh na tunahimiza kuhifadhi “az-Zaad”[1] kwa sharti mwanafunzi atambue dalili na aifuate. Hatumtii dosari yule ambaye atahifadhi matini ya ki-Fiqh kwa sharti atazame dalili zake.

Sisi tunachukia mambo ya ushabiki na tunayatupilia mbali kabisa.

Tunatilia umuhimu somo la Nahuw na Swarf na tunasoma vitabu vya adabu na vya mashairi.

Tunawalingania watu kuzirekebisha nafsi zao kuanzia ´Aqiydah zao na tabia zao na kujitahidi katika ´ibaadah.

Tunashaji´isha kuzifanyia kazi Sunnah na kuzihuisha.

Tunaonelea kwamba yule mwenye kujaribu kuleta Salafiyyah kwa njia ya ukundi kwa mtindo wa makundi ya kivyamakivyama yalioko hii leo kwamba amekosea na kwamba sisi tumejitenga mbali na mtu huyo.

Haya ni sura ya jumla yale tunayoonelea. Tunamuomba Allaah atufanye imara, atutie nguvu, atunufaishe sisi na anufaishe kupitia sisi. Kwani hakika Yeye ndiye Mwenye kusimamia hayo na muweza wa hayo. Huo ndio upambanuzi wa misingi yetu au upambanuzi wa baadhi yake.

[1] “Zaad-ul-Mustaqna´ Mukhtaswar al-Muqniy´” ya al-Hajjaawiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 23-25
  • Imechapishwa: 15/07/2020