03. Hadiyth “Mtume wa Allaah aliamka asubuhi… “

201 – ´Abdullaah bin Buraydah amesimulia kutoka kwa baba yake aliyesema:

:أصبحَ رسولُ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – يوماً فدعا بلالاً، فقال

“يا بلال! بِمَ سبقتني إلى الجنّة؟ إنني دخلتُ البارحةَ الجنّةَ فسمعت خَشخَشَتكَ أمامي؟”

فقال بلالٌ: يا رسول الله! ما أذَّنتُ قَطُّ إلا صلّيتُ ركعتين، ولا أصابني حَدَثٌ قط إلا توضَّأت عنده. فقال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

.”بهذا”

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamka asubuhi akamwita  Bilaal na kusema: “Ee Bilaal!” Ni kwa kitu gani umenitangulia Peponi? Hakika mimi jana nimeingia Peponi na nikasikia nyayo zako mbele yangu.” Bilaal akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Sijawahi kutoa adhaana kamwe isipokuwa nitaswali Rak´ah mbili baada yake. Na wala sijawahi kuchengukwa na wudhuu´ kamwe isipokuwa nitaswali baada yake.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ni kutokana na hilo.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/199)
  • Imechapishwa: 01/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy