03. Hadiyth “Mnaonaje lau kungekuwa na mto nje ya mlango wa mmoja wenu… “

352 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

أرأيتم لو أن نهراً بباب أحدكم يغتسل فيه كل يوم خمسَ مراتِ هل يبقى من درنه  شئ؟ قالوا: لا يبقى من درنه شئٌ. قال: فكذلك مثلُ الصلوات الخمس يمحو الله بهن الخطايا.

“Mnaonaje lau kungekuwa na mto nje ya mlango wa mmoja wenu ambapo anaoga kila siku mara tano kungebaki chochote katika uchafu?” Wakasema: “Kusingebaki chochote katika uchafu.” Akasema: “Basi vivyo hivyo ndio mfano wa swalah tano; Allaah anafuta kwazo madhambi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/263)
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy