02. Hadiyth “Siku moja tulipokuwa tumekaa na Mtume wa Allaah… “

351 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

بينما نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذْ طلع علينا رجلٌ شديد بياض الثياب شديد سواد الشعر لا يُرَى عليه أثرُ السفر، ولا يعرفه منا أحدٌ حتى جلس إلى النبى صلى الله عليه وسلم فأسند ركبتيه إلى رُكبتيه ، ووضع كفيه على فخذيه، فقال: يا محمدُ أخبرنى عن الإسلام، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: أن تشهد أن لا إله إلا الله، وأن محمداً رسول الله، وتقيم الصلاة، وتؤتى  الزكاة، وتصوم رمضان، وتحج البيت

“Siku moja tulipokuwa tumekaa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana. Hakuwa na alama ya kuonesha kuwa ni msafiri na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake.” Akasema: “Ee Muhammad, nieleze kuhusu Uislamu!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji Nyumba.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imepokelewa kutoka kwa Maswahabah wengi katika vitabu Swahiyh na vyenginevyo.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/262)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy