252 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakaposema muadhini:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

mmoja wenu akasema:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

kisha akasema:

أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

naye akasema:

أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

kisha akasema:

أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ الله

“Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.”

naye akasema:

أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ الله

“Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.”

kisha akasema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

naye akasema:

لا حولَ ولا قوةَ إلا بالله

“Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

kisha akasema:

حيَّ على الفلاح

“Njooni katika mafanikio.”

naye akasema:

لا حولَ ولا قوةَ إلا بالله

“Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

kisha akasema:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

naye akasema:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

kisha akasema:

لا إِله إِلا الله

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

naye akasema:

لا إِله إِلا الله

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

kutoka moyoni mwake, basi ataingia Peponi.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud na an-Nasaa´iy[2].

[1] Swahiyh.

[2] Bi maana katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (40/155). Hadiyth imetajwa katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (1/258). Katika Hadiyth kuna ishara juu ya kwamba muadhini anatakiwa kusema:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

mara mbilimbili, na si mara moja, kama wanavofanya waadhini katika baadhi ya miji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/220-221)
  • Imechapishwa: 07/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy