02. Hadiyth “Mtapomsikia muadhini, basi semeni mfano wa anayosema… “

251 – ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

إذا سمعتم المؤذنَ فقولوا مثلَ ما يقولُ، ثم صلُّوا عليَّ؛ فإنه من صلّى عليَّ صلاةً صلّى الله عليه بها عشراً، ثم سلُوا الله لي الوسيلةَ؛ فإنّها منزلةٌ في الجنة لا تنبغي إلا لعبدٍ من عباد الله، وأرجو أنْ أكون أنا هو، فمَن سأل الله لي الوسيلة حلّت له الشفاعةُ

“Mtapomsikia muadhini, basi semeni mfano wa anayosema. Kisha niswalieni. Kwani hakika yule ambaye ataniswalia mara moja, basi Allaah atamsifu kwayo mara kumi. Kisha niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة). Hiyo ni ngazi Peponi ambayo haimstahiki isipokuwa moja miongoni mwa waja wa Allaah na mimi nataraji kuwa ndiye. Yule ambaye ataniombea kwa Allaah Njia basi utamthubutikia uombezi wangu.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/220)
  • Imechapishwa: 07/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy