02. Wasifu mfupi wa Abu Haniyfah, Abu Yuusuf na Muhammad bin al-Hasan

Abu Haniyfah alikuwa Imaam an-Nu´maan bin Thaabit al-Kuufiy. Alizaliwa mwaka wa 80 na akakutana na Maswahabah wengi. al-Khatwiyb amesema:

“Alimuona Anas bin Maalik.”

Alikuwa (Rahimahu Allaah) mwanachuoni, mwenye kuipa nyongo dunia, mfanya ´ibaadah, mwenye kujichunga na mchaji Allaah. Alikuwa ni mwingi wa unyenyekevu na mwenye kujidhalilisha mbele ya Allaah (Ta´ala).

Alifariki mwaka wa 150. Mwaka huohuo ndio kazaliwa Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah).

Abu Yuusuf alikuwa ni imamu mairi na mujtahid wa moja kwa moja Ya´quub bin Ibraahiym al-Answaariy al-Bajaliy. Alizaliwa mwaka wa 113 na akasoma elimu kutoka kwa Imaam Abu Haniyfah na wengineo. Kuna wengi ambao walichukua elimu kutoka kwake, mmoja wao ni Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). ar-Rashiyd alimpa kazi ya ukadhi na akashikamana nayo mpaka alipokufa mwaka wa 183. Wakati Abu Yuusuf alipofariki Haaruun ar-Rashiyd alimpa kazi hiyo mtoto wake Yuusuf mpaka alipofariki. Wakati liliposindikizwa jeneza la Abu Yuusuf watu walisema:

“Fiqh imekufa.”

Fiqh haikufa

lakini imetoka kwenye kifua cha mtu na kwenda kwenye kifua cha mwengine

Muhammad bin al-Hasan bin Farqad ash-Shaybaaniy ambaye alipewa kazi ya ukadhini na ar-Rashiyd. Alisafiri pamoja na ar-Rashiyd kwenda Khuraasaan na akafariki Rayy na akazikwa huko.

Baba yake alikuwa miongoni mwa wanajeshi wa Shaam. Alifika Waasitw mwaka wa 132 na huko ndipo akamzaa Muhammad.

Alikulia Kuufah na akachukua elimu kutoka kwa Abu Haniyfah, Maalik, Abu Yuusuf na wengineo. Akiwa mtoto wa miaka ishirini alikuwa anatoa darsa katika msikiti wa Kuufah. Ibraahiym al-Harbiy amesema:

“Nilisema kumwambia Imaam Ahmad: “Ni wapi umetoa mambo haya ya kina?” Akasema: “Kutoka kwenye vitabu vya Muhammad bin al-Hasan.”

Alifariki (Rahimahu Allaah) mwaka wa 189. as-Sam´aaniy amesema:

“Muhammad bin al-Hasan na al-Kasaa-iy walikufa siku moja huko Rayy.”

Inasemekana kwamba ar-Rashiyd alikuwa akisema:

“Niliizika Fiqh na kiarabu huko Rayy.”

Muhammad bin al-Hasan alikuwa ni binamu yake na al-Farraa´, imamu anayejulikana kwa sarufi na lugha. Allaah awarehemu wote.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Maaniy´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 15-17
  • Imechapishwa: 10/11/2021