Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tambua – Allaah akurehemu –

MAELEZO

Neno ”tambua” maana yake yakinisha na uamini kwa kukata. Elimu ni hukumu ya kutoka akilini ya kukata. Ni yale ambayo mtu ana yakini nayo. Kwa sababu vinavyodirikiwa ni aina nne:

1 – Elimu.

2 –Shaka.

3 –Dhana.

4 – Ufikiriaji.

Kitu ambacho mtu ana yakini nacho huitwa kuwa ni elimu. Kitu ambacho mtu ana mashaka nacho na anasitasita, ikiwa ujuzi na mashaka vyote viwili vinalingana na hakuna upande wowote katika pande hizo mbili ambao una nguvu zaidi kuliko mwingine huitwa kuwa ni shaka. Ikiwa kuna jambo la kusitasita kati ya ujuzi na mashaka, basi ule upande wenye nguvu zaidi huitwa dhana na ule upande usiokuwa na nguvu zaidi huitwa ufikiriaji.

Mtunzi wa kitabu amesema:

“Allaah akurehemu.”

Malengo ni kukuombea du´aa. Maana yake anakuombea Allaah akurehemu. Huku ni katika kukutakia kwake (Rahimahu Allaah) kheri. Anakufunza na anakuombea rehema. Wanazuoni ndio watu wanaowatakia watu kheri zaidi. Hivo ndivo alivosema Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah”:

“Wanawahuisha kwa Kitabu cha Allaah wale waliokufa na wanawafanya kuona kwa nuru ya Allaah wale vipofu. Ni wangapi waliokuwa wameuliwa na Ibliyswamewahuisha! Na ni wangapi waliokuwa wamepotea wamewaongoza! Ni uzuri uliyoje athari zao kwa watu na ni ubaya uliyojeathari za watu dhidi yao!”[1]

Bi maana athari za wanazuoni kwa watu ni nzuri. Kwa sababu wanawafunza, wanawaongoza na wanawaamsha kutoka katika ujinga. Upande wa pili watu wanawaudhi.

Ibn-ul-Qayyim amesema kuhusu wanazuoni:

“Wenye kudangana huongoka kupitia wao, waliosimama wakatembea kupitia wao,  wenye kupuuza wakanyooka kupitia wao, waliokata tamaa wakapata matarajio kupitia wao na wanyonge wakapata nguvu kupitia wao.”[2]

[1]Tazama “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah”, (01/55).

[2] Madaarij-us-Saalikiyn (03/284).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 30/01/2023