02. Tunachukua elimu kwa wanachuoni hawa na mfano wao

Tunaona kuwa ni jambo la lazima kufungamana na wanachuoni wa ki-Salaf. Katika karne hizi za mwisho wanawakilishwa na maimamu wa Da´wah an-Najdiyyah (Rahimahumu Allaah) na wale walioathirika nao katika wakati wao na baada yao.

Tunachukua elimu kutoka kwa wanachuoni wetu wanaotambulika kwa Sunnah ambao hawakuchafuka kwa uchafu wa Bid´ah wala matamanio. Himdi na neema zote ni stahiki ya Allaah kuona ni wengi. Miongoni mwao ni:

1- Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz.

2- Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy.

3- Shaykh Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn.

4- Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan.

5- Shaykh ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan.

6- Shaykh Swaalih bin ´Abdir-Rahmaan al-Atram.

7- Shaykh ´Abdul-Muhsin Hamad al-´Abbaad.

8- Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Abdillaah Aalush-Shaykh.

9- Shaykh Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd.

10- Shaykh Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan.

Wako wengine wengi miongoni mwa ndugu zao wanachuoni ambao ni mfano wao.

Sisi hatuonelei kuwa wamekingwa na kukosea. Wao ni watu na wanapitikiwa na makosa na kusahau kama yanavyowapitikia wengine.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 13/07/2020