01. Misingi ndio yenye kuamua Salafiy mkweli na mwongo

Misingi hii ndio ambayo itampambanua Salafiy wa kweli na yule ambaye ni mwenye madai mwongo.

Wako baadhi ya watu ambao wanajinasibisha na Salafiyyah lakini ukweli wa mambo wako mbali kabisa. Ashaa´irah wanadai kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; lakini wamesema uongo. al-Ikhwaan al-Muslimuun wanadai kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, lakini kuna tofauti kubwa kati ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na mfumo wao na yale wanayopita juu yake.

Misingi hii nitakayoitaja walinganizi wote wa mfumo wa Salafiy wameafikiana juu yake hapo kale na hivi sasa. Lakini kabla sijataja misingi hii na kuibainisha ubainifu wa kutosheleza, nasema: Salafiyyah tunayolingania kwayo sio kama makundi ya Kiislamu na kivyama yaliyoko hii leo. Salafiyyah ndio kundi la waislamu. Kila ambaye ataitakidi ´Aqiydah ya Salafiyyah na akashikamana nayo kiuhalisia, basi huyo ni Salafiy. Hatupambanui kati ya mmoja na mwengine.

Sisi hatuna mafungamano zaidi ya mafungamano na watawala na wanachuoni wetu. Hatufichi kitu kwa yale tuliyonayo. Yale ambayo tukoemo yameandikwa ndani ya vitabu na yanasikika kwenye kanda. Hakuna usirisiri wala hatuna mtandao usiyokuwa wa mtawala.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 13/07/2020