2 – Madhambi ambayo kuna kujitenga mbali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema ni pamoja na:
“Yule mwenye kutughushi basi si katika sisi.”[1]
“Si katika sisi yule mwenye kubeba silaha dhidi yetu.”[2]
“Si katika sisi yule asiyewahurumia wadogo wetu.”[3]
[1] Muslim (101) kupitia kwa Abu Hurayrah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa tamko lisemalo:
“Yule mwenye kubeba silaha dhidi yetu si katika sisi, na yule mwenye kutughushi si katika sisi.”
Yeye pia ndiye ambaye amepokea sehemu yake ya kwanza kupitia kwa Ibn ´Umar na Abu Muusa.
[2] Muslim (101).
[3] Ahmad kupitia kwa Ibn ´Umar kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Haakim ameisahihisha kwa mujibu wa sharti za Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 70
- Imechapishwa: 29/06/2023
- Taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy