Ndani yake kunaitakasa na kuisafisha nafsi kutokamana na mchanganyiko na maadili mabaya. Swawm inafanya zile njia za shaytwaan kuwa nyembamba mwilini mwa mtu. Kwani shaytwaan anatembea ndani ya mwanadamu kama ambavo damu inatembea kwenye mishipa. Kwa hivyo anapokula au akanywa basi nafsi yake inajitanua juu ya matamanio, matakwa yake yananyongeka na hamu yake ya ´ibaadah inakuwa chache. Kufunga ni kinyume na hivo.

Kufunga kunamfanya mtu kuipa kisogo dunia na matamanio yake na kunamfanya mtu kuwa na shauku ya Aakhirah.

Swawm inamfanya mtu kuwa na huruma juu ya wale masikini na kuhisi maumivu yao kutokana na yale maumivu ya njaa na kiu anachokipata mfungaji.

Kwa sababu maana ya kufunga katika dini ni kule kujizuia kwa manuizi kutokamana na vitu vinavyohisiwa kama vile kula, kunywa, kufanya jimaa na vyenginevyo vilivyopokelewa katika Shari´ah. Yanafuatia hayo kujizuia kutokamana na maneno ya upuuzi na ufuska.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/374)
  • Imechapishwa: 22/03/2021